logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jua Cali Afichua Siri Ya Katika Usanii Kwa Miaka Nyingi

Jua Cali Afichua Siri Ya Katika Usanii Kwa Miaka Nyingi

image
na

Habari01 October 2020 - 16:18
jua-cali
Msanii aliyebobea kwa mtindo wa Genge humu nchini, Jua Cali leo alizuru studio za Radio Jambo katika kitengo cha waliobobea ambapo aliungana na watangazaji, Gidi na Ghost.

Jua Cali ambaye amekuwa katika ulingo wa usanii kwa zaidi ya miaka kumi na mitano amekuwa mojawapo ya wasanii, thabiti zaidi ikilinganishwa na wenzake ambao aidha hawakufua dafu au walikata tamaa.

Msanii huyu ambaye jina lake rasmi ni Paul Julius Nunda, anatambulika kwa nyimbo zake kama; 'Bidii Yangu' 'Nyundo' 'Kwaheri' na pia 'Baba Yao', tangia alipojitosa katika ulingo wa usanii nyimbo ambazo zilimwezehsa kupaa juu zaidi na kunyakua tuzo chungu nzima.

Lakini siri yake Jua Cali ni ipi iliyomwezesha kudumu katika muziki na kuwa na mashabiki chungu nzima?.

Hilo ndilo lililokuwa swala kuu kwake ambaye pia ndiye mwanzilishi wa studio za muziki almaarufu 'Calif Records', swali ambalo liliwafungua wengi macho na pia fikra haswa wasanii wanaojitokeza sasa hivi.

"Siri ni rahisi sana." Alijibu Jua Cali. "Penda kazi yako. Yaani kuwa tu na shauku ya muziki, heshimu muziki na muziki utakuheshimu.

Mimi toka nianze sanaa muziki ndio umekuwa nambari moja, umaarufu na mambo ya fedha huja baadaye" Alieleza msanii huyo.

Baadhi ya mambo aliyoangazia pia ni kuhusu kanda mpya anayotayarisha kuzindua mwaka ujao itakayohusisha nyimbo kama; 'Safsana' na 'Muoto sana' pamoja na muziki ambao anadhani kuwa ndio bora zaidi kwake.

Skiza uhondo katika kanda ifuatayo.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved