Rasanga alielezea kuwa kusheheni kwa ugonjwa wa ukimwi katika kaunti ya Siaya kumechangiwa na utamaduni wa kuwaridhi wajane.
Aliongezea kuwa anapania kutenda fedha ambazo zitatumika kama hazina ya wajane ili kuwasaidia kufungua biashara ili kujikimu kimaisha na kuwasaidia kujiepusha na utamaduni wa kuridhiwa kwa mjibu wa usaidizi.
Aidha haya yanajiri baada ya baraza la kuthibiti ugonjwa wa ukimwi kubaini kuwa kaunti ya Siaya ni ya tatu nchini katika usabazaji wa ugonjwa wa ukimwi.