Mbunge wa Tigania East Mpuri Aburi na seneta wa Meru Kiraitu Murungi wamekanusha madai kwamba watamtumia mganga kuhakikisha kwamba Kiraitu anashinda kiti cha ugavana katika uchaguzi wa mwaka huu .
Wakizungumza katika hafla tofauti wawili hao wamevishtumu vyombo vya habari kwa kuongeza chumvi utani uliotolewa na bwana James Mugambi Barongo al maarufu ‘Kaana Ka Njoka’ aliyesema ana nguvu za kiganga kumsaidia kiraitu kushinda kiti hicho .
Mugambi aliwatishia wale ambao hawatompigia kiraitu kura kwamba wataaga dunia. Lakini sasa wamejitenga na vitisho hivyo na kuviita ‘utani’ wa ‘kuwachekesha watu’ .