logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO: Niligundua Mume Wangu Ana Mke Na Watoto Baada Ya Miaka Kadhaa

PATANISHO: Niligundua Mume Wangu Ana Mke Na Watoto Baada Ya Miaka Kadhaa

image
na

Habari01 October 2020 - 18:38
Bi. Sophie alituma ujumbe akisema "Naomba mnipatanishe na mume wangu Silas, ambaye tulikosana baada ya kugundua kuwa alikuwa amezaa watoto wawili maeneo ya Turkana."

"Mume wangu alikuwa polisi na alikuwa maeneo ya Turkana kwa miaka kumi kikazi mahala alipokuwa ameoa bila kuniarifu. Siku moja nilikuwa kwake na mwanamke mwingine akanivamia akiniambia nitoke kule kwani yeye ndio mkewe. Hapo nikamtuliza nikimuambia kuwa jambo la busara ni kumngoja mwanaume huyo arejee ili asuluhishe yote. Baada ya kurudi alikana kuwa hamjui mwanamke yule lakini nahisi nilipo ondoka, wawili hao walirudiana," alieleza Sophie.

"Sasa juzi alihamia Nairobi kutoka Turkana na nikama alibeba mwanamke mwingine kwani nilipiga simu na mwanamke mwingine ndiye aliyejibu simu. Pamoja tuna watoto watatu lakini ndiye aliyewachwa na watoto huku nikiishi kivyangu," aliongeza.

Alipopigiwa simu bwana Silas alisema kuwa tendo la Sophie kumchomea mavazi ni jambo mbaya sana kulingana na mila na desturi zao.

"Hilo jambo ni kubwa sana kwani inamaanisha kuwa nikama ameniua nikiwa uhai, ni jambo mbaya sana,"alijieleza huku akisema kuwa swala lake kuwa na mke na watoto wengine halina msingi wowote na kesi hii.

Pata uhondo kamili hapa.

&feature=youtu.be


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved