logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO: Mimi Nampenda Mume Wangu Heri Hata Niende Kwake Aniue

PATANISHO: Mimi Nampenda Mume Wangu Heri Hata Niende Kwake Aniue

image
na

Habari02 October 2020 - 13:43
Karen mwenye umri wa miaka 22, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe Peter.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya mwaka mmoja na hawajajaliwa mtoto bado.

Kulingana na Karen; "Tulikosana mnamo tarehe 22 mwezi wa saba. Mimi tulivyooana na mume wangu aliniwacha nyumbani na mama mkwe naye akasafiri kikazi hadi Ngong. Juzi tukakosana na mama mkwe na nikampigia mume wangu simu kumueleza kuwa nilihitaji nauli ili nisafiri hadi nyumbani.

Alinitumia na niliposafiri nikarudi baada ya siku kadhaa lakini mama mkwe akanikanya kufika katika boma lake na hapo nikasafiri hadi kwa ndugu yangu."Alieleza bi Karen huku akifichua kuwa kuna mwanadada fulani aliyempigia simu akidai kuwa ni mpenzi wa bwana yake.

Basi nilimpigia bwanangu kumuuliza kuhusu hayo na akakiri kuwa yule ni mpenzi wake sasa nashindwa ni nini nilimfanyia na vile nampenda.

Mimi nampenda bwanangu na hata akinikataa nitaelekea hadi kwake aniue heri hata nilale kwa mlango. Mimi nampenda sana bwanangu." Alisema.

"Unajua kwa hii dunia kitu kibaya ni kuoa mwanamke halafu atusi mama mzazi." Alidai Peter.

Unajua hata miezi mitatu haijapita tangia baba mzazi alifariki na hata machozi hayajaisha na mke wangu amemtusi." Alieleza akisisitiza kuwa bado anampenda mkewe na anafahamu kuwa mkewe anampenda.

Mimi nakupenda sana kwani wewe ndio bwanangu milele!" Alisema Karen huku akisema kuwa atarekebisha tabia zinazoudhi familia ya bwanake.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved