Mwanamume mwenye umri wa miaka 32 umeuliwa na umma kwa kuteketezwa moto baada ya kudaiwa kumwuuwa kwa kumdunga kisu shingoni mpenziwe mwenye umri wa miaka 37 katika kijiji cha Mwanandunyi huko Tausa,Voi kaunti ya Taita Taveta.
Kulingana na jamaa za mwanamke aliyeuawa ni kuwa, mwanaume huyo kutoka Kisii alikuja kumtembelea mpenzi wake wakati wa Krismasi kabla ya ugomvi kuzuka kati yao hapo jana.
Kamanda wa polisi kaunti ya Taita Taveta Fredrick Ochieng amedhibitisha kisa hicho na kuwashauri wanandoa kutafuta suluhu kutoka kwa wazazi wanapokosana.
Solomon Muingi
Also

