Akizungumza na wanahabari mwathiriwa ambaye ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya siyenga amesema mshukiwa David Lugalia almaarufu mia mbili amekuwa akimhadaa kwa shillingi ishirini kabla ya kumtendea unyama huo na baadaye kumuonya dhidhi ya kumueleza yeyote kabla ya kufumaniwa na mchungaji wao akitekeleza kitendo hicho.
Kisa hiki kimedhibitishwa na afisa wa watoto katika kaunti ndogo ya likuyani bi Milcah Chelagat Sitienei ambaye amesema polisi wanamsaka mshukiwa ambaye amekimbilia mafichoni kwa sasa.
-Brian Ojamaa
