logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila akutana na Maghufuli kuhusu kulinganisha masuala ya ndani

Raila akutana na Maghufuli kuhusu kulinganisha masuala ya ndani

image
na

Habari02 October 2020 - 00:11
raila odinga
Kinara wa ODM aliweza kukutana na rais wa Tanzania John Pombe Maghufuli katika nchi ya Tanzania. Kupitia mtandao wa kijamii wa twitter Raila alisema walieza kujadili kulinganisha masuala ya ndani.

"Niliweza kupatana na rafiki yangu Rais  Maghufuli asubuhi," Raila alisema.

Raila ambaye ni (AU envoy for infrastructure) aliweza kuudhuria mchezo wa mwisho wa sportpesa huko Dar es salaam jumapili ambapo Kariobangi Sharks waliichapa timu ya bandari 1-0 kwa kujiinua kidogo.

Hapo awali Raila aliweza kupeana mfano na rais wa Tanzania John Maghufuli, ambaye alisema aliweza kufanya jitihadakubwa katika kutokomeza ufisadi, kando na nchi ya Kenya.

Ambayo ilichukua hatua kali.

Raila alivunja kimya chake baada ya kuonekana na mashaka ya hali yake ya kiafya katika uwanja wa Dar es salaam, wakati wa kuzawadiwa kwa timu ya sharks.

Jambo lililoleta mjadala katika mitandao ya kijamii. Lakini baada ya masaa machache  Raila alisema kuwa yuko salama katika mtandao wake wa kijamii wa twitter.

"Wapendwa wananchi wa kenya na marafiki,niko salama na afya yangu ni nzuri,asanteni kwa kujali," Raila aliongea.

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved