Mzee Abdul alimtaliki mkewe miaka ya awali kijana huyu akiwa kidato cha kwanza. Naseeb alitangulia kwa kusema kuwa ubaridi unaonekana kati yao na baba mzazi umechochewa na kutokua pamoja kwa kipindi kirefu.
“Kiukweli siwezi kusema nina ukaribu na mzee. Hatujakuwa na bond kubwa naye ila mimi sina matatizo naye…tukiwa kuna issue tutakutana naye tuongee” Diamond alisema katika mahojiano.
Kwa upande mwingine anaona kuwa babake anamweka katika kicheko kwa watu wengi hususan wapinzani wake anapoonekana kama hamsaidii mzazi.
Babake alimwomba msamaha na wote kuonekana wameridhiana katika mazungumzo yao
“Kama nimekukosea naomba unisamehe na ujaribu kuangalia utanisaidia vipi mimi babako.”
Diamond alionya kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vinavyomtumia babake kwa maslahi yao na hawamsaidii. Mkali huyu wa kibao kipya The one alimaliza kwa kuomba msamaha.
“Well mimi siwezi kusema nina matatizo na babangu. Naamini utofauti wake na mama unafanya tuwe hatuna ukaribu…Naomba anisamehe pia kwa sababu sijui akiwa na mama walikosana kwa misingi gani.”