logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nini humfanya mtu kupiga punyeto? waraibu waeleza

Nini humfanya mtu kupiga punyeto? waraibu waeleza

image
na

Habari02 October 2020 - 11:15
Akiwa na umri wa miaka 22, Hance* hangeweza kumkaribia msichana kwa hofu ya kukataliwa. Kwa sababu ya kukosa kujiamini, alianza kujitimizia hisia zake za ngono.

“ Uso wangu ulichomeka nikiwa na umri wa miaka 12 na kuharibiwa kabisa. Nilishindwa hata kujitambua mwenyewe na kuamini kwamba nilikuwa na sura mbaya. Nilifikiri hakuna mwanadada angelinikubali,” alisema.

Aliendelea kuzama katika hali ya kutojiamini na akaanza kusoma nakala za ngono ili kung’amua haja ya ngono iliokuwa “ikichemsha damu yake” na mabadiliko katika mwili wake.

“Riwaya za ngomo nilizopata kwa marafiki zangu zilikuwa zaniliwaza hisia zangu za kimwili,” Hance alisema kwa sauti ya chini.

Vile aliendelea kusoma nakala za ngono, ndivyo msukumo wake wa kushiriki tendo hilo ulipozidi na kumsukuma katika dimbwi la punyeto.

“Nilijimalizia hisia zangu za ngono chumbani nikiwa katika shule ya mabweni na kuhisi vyema baada ya kitendo hicho,” alieleza.

Baada ya “kujichezea gitaa” mwenyewe kwa muda wa miaka minne, alianza kujitenga na watu akitafuta mahali pa kujificha ili asipatwe na wenzake akijipiga punyeto.

Kila mtu alianza kuhoji tabia zake na mienendo yake kutosongea wasichana, lakini jibu kila mara lilikuwa “Mimi siko hivyo”.

Akilini mwake, alihisi kuwa uso wake uliochomeka ulikuwa sababu kuu yake kujitenga na wasichana, lakini hii ilisalia siri yake.

Mara nyingi, Hance alisema vile marafiki zake walimkejeli kuhusu sura yake iliyoharibika, na kudhalilisha utu wake na ndivyo alizidi kutojikubali.

Akiwa katika shule ya upili alijaribu kumsongwa msichana waliyekuwa wamesoma naye katika shule ya msingi, msichana huyo alimpuuza na kumwangalia kwa madharau.

“ Hilo liliniuma sana. Wale niliokuwa naita marafiki walikuwa sasa wanajitenga nami na kumtumbukiza hata zaidi katika tabia za “kujipepeta”. Hii iliniepushia hofu za dunia,” Hance alisisitiza.

Kwa raha zake

Baada ya kuingizwa kwa punyeto na mpenzi wake wa mbali, Anita alijipata katika uraibu wa tendo hilo na vita vya kujinasua kutoka minyororo ya uraibu huo.

“ Alikuwa anaishi mbali name na punyeto ilinipa raha niliokuwa nahitaji,” Anita alisema.

Brian*,baba ya watoto wawili alijipata katika hali ya “kujipakulia raha mwenyewe” baada ya mke wake kugonjeka na hakutaka kutembea nje ya ndoa.

Miezi miwili akipiga punyeto, mkewe alipona lakini alikuwa tayari amezama katika kisima cha punyeto na aliendelea kufanya hivyo wakati mke wake haoni.

Miaka miwili baadaye mkewe aligundua kwamba mumewe alikuwa ameanza kupoteza hamu ya tendo la ndoa.

“ Mke wangu hakuonekana mrembo tena, sikupendezwa na mwanamke yeyote. Nilianza kujiutenga, hali hii ilimdhuru sana mke wangu kimawazo,” Brian aliongeza.

Brain alimweleza mke wake shida yake na kumpeleka kwa mtaalam aliyemsadia kurejelea hali yake ya kawadia ya unyumba.

UKWELI KUHUSU PUNYETO

Inaaminika kwamba ni vijana pekee walioathirika sana na punyeto lakini takwimu zaonyesha kuwa uraibu huu unaathiri watu wote, bila kujali rangi, umri na jinsia. Ni vigumu kueleza nani anapiga punyeto zaidi kuliko mwingine.

Punyeto huleta uraibu na vile unavyoendelea kufanya tendo hilo ndivyo unavyo karibia uraibu wake.Uraibu huu una athari nyingi sana sawia na uraibu wa kucheza kamari au unywaji wa pombe.

Utafiti uliyofanywa na taasisi moja nchini Amerika kwa watu wa kati ya umri wa miaka 14 hadi 17 ulionyeshesha kwamba, asilimia 74 ya wanaume na asilimia 48 ya wanawake walikiri kupiga punyeto.

Suluhu

Ili kujikwamua kutoka minyororo ya punyeto, kwanza unafaa kubaini ni jambo lipi lilikuchochea kujipata katika hali hiyo. Suluhisho litatokana na kutatua kiini.

Unafaa pia kutafuta usaidizi kutoka kwa wataalam.

Unafaa kuacha kutazama video za ngono na kutafuta njia mbadala za kushughulikia hisia zako za ngono.

NA FAITH NYASUGULA


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved