logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Saumu Ameona! Patana na Bibi Mrembo wa Seneta wa Lamu Anwar Loitiptip

Saumu Ameona! Patana na Bibi Mrembo wa Seneta wa Lamu Anwar Loitiptip

image
na

Habari02 October 2020 - 11:14
Seneta wa Lamu, Anwar Loitiptip aliwaacha wengi vinywa wazi baada ya kumtambulisha Saumu Mbuvi (mtoto wa Mike Sonko) kama 'mchumba wake'.

Akiongelesha vyombo vya habari kutoka hospitali ya Aga Khan ambapo amelazwa, Anwar alisema;

''TULIKUWA NDANI YA GARI MAHALA PA KUREJESHA MAGARI KABLA YA MCHUMBA WANGU (SAUMU) KUTAKA KUENDA KWENYE CHUMBA CHA KUJISAIDIA. ALIPOFIKA HAPO, WANAUME WAWILI WALIMFUATA NA KUFUNGA MLANGO HUO. WALIRARUA BLAUZI YAKE NA KUTAKA KUMBAKA ILA ALIPIGA MAYOWE NA KUOMBA USAIDIZI.''

 Mwaka wa elfu mbili kumi na saba, seneta Anwar kwenye mahojiano na The Nairobian alikiri kuwa alikuwa anampenda Sophie Mohammed, Afisa wa Polisi wa Utawala.

Aliwakemea wanawake waliomtamani, ambao walitaka kuonja kipande chake.

''KWA WALE MLIOKUWA MKINIMEZEA MATE MMECHELEWA. NIMECHUKULIWA NA NIMEKUWA NIKIMUONA KIMAPENZI SOPHIE KWA MIAKA MITATU SASA. YEYE NI KILA KITU NILICHOTAKA KWA MWANAMKE, KWA KWELI, SIWEZI MCHAGUA MWANAMKE YEYOTE DHIDI YAKE. NAJUA KWAMBA KUWA MTU MASHUHURI INA VIKWAZO KAMA KUPAMBANA NA WATU WANAO FUATILIA MAISHA YAKO , ILA ITAWABIDI WAJARIBU SENETA MWINGINE KWA KUWA SIKO KWENYE SOKO SASA.''

Sophie Mohammed, ambaye anahusishwa na benki ya mtaa huko Thika alipata umaarufu baada ya picha yake kusambaa. Hali hii ilimuwezesha ashinde cheo cha  's3xiest cop' kwa macho ya wananchi.

Katika mahojiano na gazeti hilo, askari huyu mrembo alisema;

''KATIKA HARAKATI ZA KILA SIKU, HUWA NAWAKANA KATI YA WANAUME KUMI NA KUMI NA TANO AMBAO WANANITAKA.''

Swali sasa ni, je Anwar na Sophie walivunja uhusiano wao? Mbona Saumu na Anwar walishambuliwa?

Saumu na Anwar walikuwa wamemaliza kuona mechi ya mwisho ya ligi ya mabingwa kwenye eneo la Memphis lounge karibu na chuo kikuu cha USIU wakati wa shambulio hilo.

Seneta huyu anauguza katika hospitali hiyo mjini na baadhi ya picha zake akiwa hospitalini zi hapa chini.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved