Alai amejipata matatani baada ya tume ya Uwiano na maridhiano kutangulia kumsihi aziondoe picha hizo katika mitandao ya kijamii lakini akapuuza . Katika kinachothibitisha msemo aliye juu mngoje chini ,Alai hajaonewa huruma na wengi wanaomponda huku wengine wakimrejesha nyuma kumkumbusha kuhusu ukosoaji wake mkali dhidi ya kinara wa ODM Raila Odinga .
Hata hivyo baadhi ya wanamtandao hawajapendezwa na hatua ya polisi kuiweka nambari ya simu ya Alai hadharani katika kibango alichopigwa nacho picha .
