logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pwani hadi Nairobi: Vyuo vikuu vyenye malango ya kupendeza

Pwani hadi Nairobi: Vyuo vikuu vyenye malango ya kupendeza

image
na

Burudani02 October 2020 - 02:01
Kama wewe ni mwanafunzi wa chuo kikuu au una umakini wa hali ya juu, utagundua kuwa vyuo vikuu kadha wa kadha nchini vina mienendo ya kujenga malango ya kufana na kuvutia mno.

Mtindo huu ukikumbuka ulianzishwa na chuo kikuu cha Mlima Kenya (Mount Kenya University) kabla ya chuo kikuu cha Kenyatta kujenga lango la kisasa na lenye gharama ya juu.

Isitoshe, mradi huo wa lango la chuo kikuu cha Kenyatta, ulijumuisha majengo matatu mapya ambayo iliwagharimu mamilioni ya pesa.

Miaka kadhaa baadae, mtindo huu umegeuka na kuwa kama mashindano kati ya vyuo hivo huku kila mmoja akitaka kuonesha ubabe wake katika uwanja wa ubunifu.

Vyuo vingine vikuu ambavyo vimefuata mtindo huu wa kisasa ni chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT, Juja), chuo kikuu cha Pwani, chuo kikuu cha Egerton, chuo kikuu cha Kabianga, Kericho, na mengineo.

Tazama picha za baadhi ya vyuo hivi.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved