logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Barry otieno achaguliwa kama mkurugenzi mkuu wa FKF

Barry otieno achaguliwa kama mkurugenzi mkuu wa FKF

image
na

Michezo02 October 2020 - 10:56
Aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka hapa nchini Barry Otieno amechaguliwa kama mkurugenzi mkuu wa tume hio baada ya Robert  Muthomi kujiuzulu.

Robert Muthomi alijiuzulu kwa muda ili kutoa nafasi kwa uchunguzi kuendelezwa dhidi ya madai ya kuingilia uhamiisho wa mshambulizi wa sofapaka John Avire kuelekea nchini misri.

Mwenyekiti wa shirikisho la FKF humu nchini Nick Mwendwa alisema kuwa watahakikisha haki imetendeka kwa pande zote mbili na iwapo Robert atapatikana na makosa basi itamlazimu apigwe kalamu.

"Shirikisho la FKF limekuwa na mkutano wa ghafla na ni wazi kuwa majukumu yote ya shirikisho lazima yaendelezwe licha ya jambo lipi kutokea.

Kufuatia matukio hayo kamati kuu imemchagua Barry Otieno kuwa mkurugenzi mkuu wa shirikisho hili kwa muda," Nick mwenda akizungumza na vyombo vya habari hio jana ndani ya Kandanda House.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved