Hafla hii ilitarajiwa kufanyika jana ila haikuwezekana kwa ukosefu wa idadi inayotosha ya makuhani.
Sarah na Bernard walikuwa wametafuta makuhani 8 kiwango kidogo cha wanaotakikana.
Soma hadithi nyingine:
Jaji wa mahakama kuu Stella Mutuku alikuwa ametoa amri kuwa mjane Sarah apelekwe na maafisa wa usalama hadi makaburi ya wayahudi saa nane leo.
Mazishi yatakuwa ya faragha sana na yatafuata mila na itikadi za dini ya wayahudi.
Murgor alitangaza jana kuwa hafla hii itakuwa leo saa nane unusu.
Soma hadithi nyingine:
“Mazishi ya Tob Cohen yameahirishwa hadi kesho (Leo) saa nane unusu. Ni makuhani 8 kati ya 10 waliopatikana na Rabbi kwa mujibu wa itikadi za wayahudi."
“Tutafuta ugeuzi wa amri hiyo ya Sarah kuwepo. Hii kwa sababu amri tuliyonayo ilikuwa ya jana."
Jaji Stella Mutuku alitoa amri hiyo baada ya wote wanaohusika kukubaliana awe katika hafla hiyo.
Naibu wa DPP alihoji kuwa haoni tatizo Sarah kushuhudia mazishi ya mmewe.
Soma hadithi nyingine:
"Itikadi za mazishi zitakwenda sawa na mila za wayahudi na zitaendeshwa na viongozi wanaohusika wa jamii hiyo” Amesema Ombeta.
Kwa mujibu wa Murgor na Cliff, DPP,DCI na viongozi wa idara ya mahakama wameombwa na Sarah na Gabrielle kuendesha hafla hiyo.
Mwili wa bilionea huyu ulipatikana wiki iliyopita Ijumaa baada ya kupotea kwa wiki 8.
Ulikuwa umefungwa mara kadhaa ndani ya mifuko ya plastiki.
Cohen aliripotiwa kutoweka kutoka boma lake la Lower Kabete jijini Nairobi mnamo Julai 19 na 20.
