Vilevile, ingawaje makosa makuu kama ya mauaji kiapo chake huwa kumuua mhusika, kulingana na sheria ya Kenya, kiapo hiki kimetupiliwa mbali.
Mwezi uliopita, mkubwa wa gereza la Naivasha bwana George Odunga alisema kuwa kulingana na sheria ya Kenya, wafungwa ambao walikuwa wamehukumiwa kiapo cha kukaa gerezani milele wanafaa kuachwa huru endapo wako karibu kumaliza kiapo chao.
Afisa mkuu wa Naivasha bwana Samuel Ruto alisema kuwa wameshaanza kufanya na kupanga vizuri zaidi ni wafungwa wepi watakao achiliwa.
Samuel alizidi kusema kuwa, mpango huu utawafanya wafungwa wengi wasife moyo kuachiliwa na pia, itasaidia sana katika kampeni za kubadilisha tabia.
“We have complied with the order to grant remission to inmates who have served two thirds of their terms but this will also depend on their past conduct,” alisema.
Akizungmza katika mechi za michezo za gerezani, Ruto alisema kuwa, kitendo hiki kitasaidia kupunguza idadi ya wafungwa gerezani.
“Apart from decongesting the prisons, it will also give inmates serving long sentences hope that one day they will rejoin their families after serving two thirds of their terms,” he said.
Awali, wafungwa wa Naivasha walimuomba Rais afutilie mbali hukumu la kutoa maisha ya mfungwa kwani walisema kuwa, watu wengi walio kule gerezani wamebadili maisha yao.
Vilevile, wafungwa walisema kuwa, kiapo cha kuwaua watu huwafanya wafungwa wakate tamaa maishani.
Willis Opondo mmoja wa wafungwa aliyehukumiwa kifungo cha maisha alisema kuwa, kiapo hiki kilimfanya apoteze hamu ya kuishi na ata kuumiza familia yake moyo sana.
Alitoa wazo kuwa,wafungwa waliofanya kiapo cha miaka 20 wafunguliwe kwani watu hawa washajua makosa yao yalikuwa yepi na kujirekebisha.
Odunga alizidi kusema kuwa, si vyema katu kwa watu waliofanya makosa haya makubwa kukosa kuachiliwa kwa madai eti hawawezi badili maisha yao.
“It is not fair to maintain that those convicted of capital offences are not entitled to have their sentences reduced on the assumption that they are incapable of reform,” Odunga alisema.
Kwa sasa,wafungwa hawa wana azimio la kuwa huru hivi karibuni.
MORE: