Maneno haya ya Aisha yanajiri huku kisa cha mauti cha mjomba kikiripotiwa Ganda katika mkutano wa ODM.
Kufikia sasa haijabainika aliyefyatua risasi hiyo.
Aidha baada ya tukio hilo Aisha ameweza kujitetea,
“Mimi nakumbuka nikifika kwa huo mkutano. Nikishuka tu nilikutana na jamaa mmoja anaitwa Agunga. Na aliniambia mwacheni huyo mama aende atafanya nini na askari wote tunao wote…”
“So mi nikashindwa askari ni utumishi kwa wote na hawawezi kutake side…”
“Nataka niseme ya kwamba kitendo ODM wamefanya sio kizuri…”
“Wale waliopanga mkutano pale wakijua kwamba campaign period ilikuwa imeisha, wao ndio wanatakiwa wakuwe held responsible…” Alifunguka Aisha
Video ya siku chache nyuma inamwonyesha mbunge huyu akitokwa na povu katika mkutano,
https://twitter.com/EngnrDan/status/1184170085558173696
Kinachomkera mama huyu ni genge la wahuni wanaokisiwa kuwa wametumwa kutoka Nairobi kuvuruga amani Malindi,
"Na nyinyi kina mama na kina baba wa Ganda. Hakuna mtu atakuja kututisha hapa..."
"Hii mambo ya ooh wakifanya hivi ooh tutaleta fujo..."
"Kuna vijana walitoka Nairobi. Waliletwa huku na vijana wengi hapa wadogo wadogo sijui kina nani kina Kali..."
"Sijui Governors Voice, sijui ukumbafu gani wanaofanya lakini nataka niwaambie ole wenu..."
"Kwa hivyo hao vijana mlitoka Nairobi na Nationa Youth Leader wa ODM habari zenu nikonazo..."
"Na kama unamangamanga hapa Ganda utuonyesha sisi kifua my friend tutadeal na wewe vizuri..." Anafoka Aisha katika video hiyo
