Munira alisafiri mpaka nchini Tanzania ili amuone Mbosso na kusema kuwa yuko tayari kufanya lolote lile mradi ampate Mbosso.
Katika mahojiano na vyombo vya habari, Munira alisema,
''Nampenda. Kuna wanaume wengi sana wanataka kunioa huku Kenya lakini siko tayari. Nilikuja kumtafuta Mbosso na niko tayari kufanya lolote lile. Nampenda sana. Nilianza kumpenda tangu wakati alikuwa kwenye bendi ya YA MOTO. Niliuza simu yangu ndipo niweze kusafiri mpaka Tanzania.'' Munira alisema.
Munira alisema kuwa, Mwanzamziki huyu alisisitiza sana arudi nyumbani na hata kumpa shillingi elfu 10,000 za Tanzania lakini yeye hataki.
''Mwishowe, nimekutanana na yeye na aliniambia atanipea fare ya kurudi nyumbani lakini mimi siko tayari kurudi nyumbani. Alinipea shillingi 10,000 ya nauli lakini sitaki.''