logo

NOW ON AIR

Listen in Live

SABABU: Shavu ya kavu ya Harmonize, asusia mkutano wa Jubilee Kibra

SABABU: Shavu ya kavu ya Harmonize, asusia mkutano wa Jubilee Kibra

image
na

Michezo02 October 2020 - 03:59
Ubuyu upo kwamba staa na nyota wa Bongo Fleva Harmonize alisusia mkutano wa chama cha Jubilee Jumapili.

Inadaiwa kuwa utaratibu ulikuwepo kwa Konde Boy kutumbuiza raia katika mtaa huo wa mabanda.

Mkutano huu uliongozwa na naibu wa rais William Ruto na mwaniaji wa chama hicho MacDonald Mariga.\

Vyama husika vinaonekana kuwekeza zaidi katika juhudi za kutwaa ushindi katika eneo bunge hilo.

Inadaiwa kuwa uongozi wa chama cha Jubilee ulikosa kumlipa staa huyu kutoka nchi jirani mpunga wake kabla kupaa ndege kusafiri Kenya.

https://www.instagram.com/p/B4Zzo7Jn19t/

Sio mara ya kwanza Harmonize kukausha shoo nchini baada ya mapromota kukosa kulipa hela.

Konde Boy alitaka alipwe kima cha Milioni 3 kabla kufungua jukwaa katika mtaa huo wa Mabanda wa Kibra.\\

Ubuyu unahoji kuwa uongozi wa chama hiki ulitakiwa kumlipa kabla kuingia nchini Jumamosi.

Mvutano umeripotiwa kuwepo iwapo kima hicho cha pesa kinatosha masaa machache atakayotumbuiza jukwaani.

Uongozi wa Harmonize ulikataa ombi la kutaka alipwe Jumatatu.

Ushindani unaonekana wa farasi wawili katika mchakato huu wa kutafuta uungwaji mkono na kumrithi marehemu Ken Okoth.

William Ruto na Raila Odinga wanaonekana kuwekeza zaidi katika misururu ya mikutano ili kuwarai raia wa mtaa huo.

Novemba tarehe 7 ndio siku ya ndovu kumla mwanawe.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved