logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO: Baba alibomoa nyumba yangu na kupeleka mabati kwa chifu

PATANISHO: Baba alibomoa nyumba yangu na kupeleka mabati kwa chifu

image
na

Habari02 October 2020 - 04:02
Gidi patanisho
Katika kitengo cha leo cha Patanisho, bwana David ndiye aliyeomba apatanishwe na babake bwana Joram akisema kuwa haelewi kilichotokea baina yao.

David alisimulia,

Mimi mamangu alikuwa na urafiki na babangu na wakati wa kwenda nyumbani hakunikubalia kwenda kwa boma la baba. Nilipoenda nikamweleza baba anipe mahali nijenge boma.

Nikamwacha mke wangu nyumbani kwa boma nililojenga la matope na baada ya wiki mbili nikaskia baba alimwambia mke wangu kuwa atampatia nauli ili ende nyumbani kwao."

David anasema alishangazwa na yale na isitoshe babake alibomoa nyumba yake saa kumi na mbili ya usiku na kumwambia kuwa mabati yake yalipelekwa kwa naibu wa chifu ili aendee humo.

Baada ya mzee Joram kukata simu yetu, David alifunguka akisema,

Labda mama wa kambo ndiye anayemshurutisha mzee anifukuze akidhani kuwa nataka kumrudisha mamangu kwa boma. Mimi nia yangu ni kujenga kwa boma ili tuishi na mke wangu."

Bwana huyu anasema kuwa hajui kama mamake na babake walikuwa na uhusiano au walioana ki rasmi na hawezi uliza. Yeye alichokitaka ni kumjua babake ili aendelee na maisha na sasa amejipata akiyumbayumba asijue la kufanya.

Je ni mawaidha yepi unayoweza mpa bwana David?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved