logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Aliyetekwa nyara' apatikana na mpenzi akijipa raha Thika Road Mall, DCI yaeleza

'Aliyetekwa nyara' apatikana na mpenzi akijipa raha Thika Road Mall, DCI yaeleza

image
na

Burudani02 October 2020 - 10:22
getlstd-property-photo
Mwanafunzi wa chuo cha ufundi cha KMTC ( Kenya Medical Training College) amejipata taabani baada ya kudanganya kakake kuwa ametekwa nyara na watu asiowafahamu.

Kulingana na kakake, dadake alimpigia simu na kusema kuwa ametekwa nyara na wahuni waliodai kitita cha Kshs 20,000 ili wapate kumwachilia huru.

Kakake alituma pesa haraka ili dadake aachiliwe.

Baada ya kutuma hela, simu ya mwanadada huyo ilizimwa ghafla.

Kakake aliwasilisha taarifa hiyo kwa maafisa wa upelelezi ili wafuatilie kisa hicho.

Cha kushangaza ni kuwa dadake alipatikana katika sehemu ya burudani TRM (Thika Road Mall) akiwa na mpenzi wake.

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1195356133537591296

Kwa mujibu wa kauli ya idara ya DCI, mwanafunzi huyu alitumia ulaghai na kumpigia kakake simu nakuripoti kuwa ametekwa nyara.

Kiwango cha pesa cha 20,000 kilitumwa ili kumuopoa kwa 'watekaji nyara dhalimu.'

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1195356136083480576

"Kufuatia madai ya utekaji nyara ya mwanafunzi wa miaka 19, KMTC, makachero wanahoji kundi la wanafunzi waliotiwa nguvuni Thika Road Mall..." DCI ilitoa kauli.

Dili hii ya ulaghai ilifanyika ili kumlaghai kakake 20,000 na simu kuzimwa ghafla baada ya pesa kutumwa.

Kakake alihisi kuwa ni jambo la busara aripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi ili kumsaidia dadake.

Kwa sasa maafisa wa polisi wanahoji kundi la watu waliokuwa katika sehemu hiyo ya burudani ili kubaini ukweli.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved