https://www.instagram.com/p/BzWHIOhg43D/
Lavalava na dadake Diamond Platnumz, Queen Darleen ni baadhi ya wasanii na ambao kasi ya muziki wao haiendi sawa na lebo hii kubwa Afrika mashariki.
Lebo hii inajivunia kuwa na wasanii wote shupavu Afrika mashariki akiwemo Diamond Platnumz, Mbosso, Rayvanny na hao wawili wanaozembea kazi.
Aidha, Boss Tale ametaja njia watakazofuata ili wang'ae kama mbalamwezi katika soko la muziki Tanzania.
“Kwenye familia za kawaida wapo watoto wenye mafanikio na ambao hawana, hivyo hivyo kwa familia ya WCB kuna baadhi ya wasanii nyota zao zimeshindwa kung’ara” Boss Tale alisema.
https://www.instagram.com/p/B4zkyIYpByd/
Tale anahoji kuwa mazingira mazuri ni jambo na ambalo linaweza likawasaidia sana wasanii hao,
“Hivyo sisi kama viongozi wa lebo tunachokifanya ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao, kama kila mmoja kumuacha na meneja wake linalobakia ni jukumu lao kuangalia namna gani wanajiongeza,” Tale.
Tale ametaja kuwa wawili hawa wana kila lolote la kufanya ili wang'ae kama wenzao,
“Kama mnavyoona, hivi karibuni Lavalava aliachia wimbo wa ‘Tekenya’. Naona kaamua kuwatekenya mashabiki, na Queen Darleen inshallah naye hivi karibuni ataachia kazi”
Harmonize alikuwa na ni staa mkubwa hata baada ya kutemana na lebo hiyo.