logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+ Video) Harmonize a-copy paste Baba Lao ya Diamond Platnumz, video mpya

(+ Video) Harmonize a-copy paste Baba Lao ya Diamond Platnumz, video mpya

image
na

Habari02 October 2020 - 04:19
diamond (1) (1)
Staa wa Bongo Harmonize almaarufu kama Konde Boy ameachilia video ya wimbo wa Kushoto Kulia.

Video hii ina nembo ya lebo yake ya Konde Gang tofauti na kazi za awali zilizokuwa na nembo ya WCB.

WCB inayoongozwa na Diamond imemlea na kumkuza Harmonize.

https://www.instagram.com/p/B5mjx1Ong_k/

 Audio ya Kushoto Kulia imefanywa na producer wawili Bonga huku video ikiongozwa na Hascan.

Idea au concept ya video inaonekana kufanana na ya Baba Lao ya Diamond Platnumz.

Katika video ya Harmonize, kuna sehemu na ambapo yupo katikati mwa watu waliojifunga buibui nyeusi.

Video ya Baba Lao ilitangulia kudondoka huku Diamond Platnumz akionekana kati ya watu waliovaa suti na kujifunga vitambaa vyeupe.

Ni juzi tu Harmonize alikuwa katika ubishi wa midundo ya UNO na mtayarishaji wa nyimbo Magix Enga almaarufu kama Beat King.

Magix Enga hatimaye alitangaza kumsamehe.

Akichapisha ujumbe kwenye Insta, Enga alitangaza kuwa walimaliza tofauti zao.

Kuna uwezekano pande mbili zilipatana baada ya ubishi kuwepo kuhusu mdundo wa ngoma hiyo.

 Katika video hiyo, Enga anasikika akiuliza maafisa hao “Mnanikamatia nini mazee kama wimbo ya Harmonize tayari iko YouTube.”

https://www.instagram.com/p/B5YZtzMpKLK/

Yote tisa, concept ni ileile.

Sio mara ya kwanza Konde Boy kutuhumiwa kumuiga Diamond ata jinsi anavyoimba na kunengua katika video zake.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved