Mwanzoni ,hukumu hiyo ilifaa kutolewa Novemba mwaka jana kabla ya kusongeshwa hadi disemba tarehe sita ,kisha tena ikasongeshwa hadi januari tarehe 10 mwaka huu .Ibrahim amekuwa katika seli moja huko New York kwa miaka mitatu akingoja hukumu dhidi yake baada ya kuhamishwa hadi Amerika kutoka Mombasa januari mwaka wa 2017 .
Mnamo Oktoba mwaka wa 2018 Ibrahim na kakake mkubwa Baktash walikiri mashtaka dhidi yao katika mahakama ya Manhattan kwa kupanga njama ya kusafirisha dawa za kulevya za heroin na methamphetamine, kubeba bunduki za rashasha na vifaa vya kusababisha uharobifu , makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya,kuwapa hongo maafisa wa Kenya ili kukwepa kuwajibikia uhalifu wao na kuzuia haki kwa lengo la kuepuka kusafirishwa hadi marekani kujibu mashtaka dhidi yao. Jaji huyo mmoja ndiye aliyemhukumu Baktash kifungu cha miaka 25 jela agosti mwaka jana .