Anasema kuwa alilelewa maisha ya taabu na baada ya wazazi wake kutengana na katika kukuru kakara za maisha alipachikwa mimba akiwa mchanga.
Baada ya hilo, alishauriwa kuwa ili kuavya mimba ile, anapaswa kunywa kikombe kimojacha mjani chai kilo moja.
"Niishauriwa kuwa majani chai yaweza toa uja uzito. Nilichukua kilo moja ya majani chai nikapika chai kikombe kimoja , harufu tu ilitorosha."
Anasema kuwa alinajisiwa na mtu ambaye hakumjua baada ya kuwekewa dawa katika kinywaji chake wakiwa isikuti kabla ya mazishi.
"Marafiki wangu walikuja kwa boma la binamu yetu kutufariji na jamaa fulani akaja na akatununulia kinywaji cha soda. Soda zilikuja zikiwa zimefunguliwa na sikujiskia hadi siku ifuatayo." Alieleza Carol.
Aliongeza,
Kuna ndugu yangu alikuwa na simba na nilipopata fahamu nilijipata huko nikiwa nahisi maumivu na nikapata nina damu. Sikushughulika sana licha ya kuhisi uchungu na nilidhani siku zangu za hedhi zimefika."
Alisema kuwa alienda mtooni na kuoga na kufua zile nguo na wakti nguo zilikauka ndipo alirudi kwa boma, na hakumwambia yeyote kwani alikuwa anaishi na nyanyake.
Carol anasema kuwa alilelewa maisha ya mateso na baba wa kambo baada ya mamake na babake kutengana.
Step grandfather pia ilifika wakati akaanza kunitumia kujiridhisha kingono. Nilipoambia mamangu mzazi nilipokea kichapo cha mbwa na sikuweza kula kwa siku tatu.Kuharibu, mwanawe alikuwa anachukua vijiti vya kiberiti kunidunga sehemu ya siri na sikuwa na wa kutegemea.
Carol ambaye sasa ana miaka 30, na mama wa watoto wawili, anasema kuwa hata baada ya kupita mtihani babake hakutaka kumpeleka shule ya upili na ilimbidi alazimishe babake ampeleke katika shule tu ya kawaida.
Nilitapika besheni mbili na baada ya siku kadhaa niliona bado tumbo iko vile vile na kwenda hospitalini nikaambiwa mtoto yuko salama.
Kwenda kwa maasai alianza kunichokora sehemu za siri na nikasema hapana. Nilivumilia na nikajifungua mimi mwenyewe bila usaidizi wa yeyote na nikajifungua msichana mrembo.
Baada ya miezi sita ya kujifungua, alipewa nafasi ya kufanya kazi Nairobi na hakujua kuwa alikuwa anauzwa kama mke wa mtu.
Waliishi na yule jamaa kwa mda wa miaka saba na mwaka wa kwanza ulikuwa wa mateso na vichapo. Isitoshe siku moja alipasuliwa kichwa kisa na maana, aliomba fedha za chakula.
Hata hivyo walitengana baada ya wawili hao kujaliwa na mtoto mmoja ambaye jamaa huwa hamshughulikii.