logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fikiria kwanza kabla ya kuanza kuishi na mpenzio - Mwanasaikolojia

Fikiria kwanza kabla ya kuanza kuishi na mpenzio - Mwanasaikolojia

image
na

Habari02 October 2020 - 04:52
Umeshauriwa kuchukua muda na kufikiria kwanza kabla ya kuanza kuishi na mpenzi wako. Mwanasaikolojia Moffat Kago anasema kuanza maisha pamoja bila ya kuwaza vizuri, kunakuweka katika hatari ya kuvunjika moyo iwapo mambo hayatakwenda kama ulivyotarajia.

Mchanganiko wa habari;

Miili ya watu 4 waliopotea kwa njia tatanishi huko Kwale hatimaye imepatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali Makindu kaunti ya Makueni. Afisa mkuu wa Haki Africa Hussein Khalid, anasema miili hiyo ilipatikana katika mbuga ya Tsavo kati ya mwezi Disemba na January.

Iwapo mtoto wako amefikia umri wa miaka miwili na mitatu na bado hawezi kuongea, basi unashauriwa kumuona daktari kwani huenda ikawa ana matatizo ya kusikia. Mtaalamu wa usemi Grace Macharia hata hivyo anasema kukosa kwao kusikia haimaanishi kuwa ni kiziwi.

Watu 46 walinusurika kifo jana walipokua wakielekea katika mkutano wa BBI huko Kitui, baada ya basi walimokuwa wakisafiria kusombwa na maji ya mto Waani. Kamanda wa polisi wa Mbooni Mashariki Agnes Omojong' alithibitisha kuwa hakuna aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho.

Magavana kutoka eneo la North Rifft wanatafuta njia mpya za kudumisha amani na usalama katika maeneo yanayokumbwa na uvamizi wa majambazi. Magavana hao wanasema kanisa pamoja na viongozi wamechangia pakubwa kumaliza mashambulizi hayo katika eneo la Kerio Valley, lakini bado kuna maeneo ambayo yanavamiwa.

Wanasema watashirikiana na viongozi wa kanisa kujenga uiano kati ya jamii.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved