Hii ni baada ya wiki zilizopita uvumi kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa uhusiano wa wawili hao una yumbayumba, uvumi huo ulienea baada ya Diamond kumuacha Tanasha Nairobi kwa hali isiyojulikana.
Kwa hakika msanii Diamond ametoa nyimbo nyingi akiwashirikisha wasanii tofauti nchini Tanzania na humu nchini, Tanasha ni mpenzi wake Diamond ambaye ametoa wimbo na yeye katika wapenzi wote ambao Diamond amekuwa nao.
Wimbo wa Gere unazungumzia jinsi watu wanaumbea kuhusu uhusiano wa mapenzi kwa watu wengine.
Cha ajabu ni kuwa Tanasha ni mwanamke wa pili kutoka humu nchini kushirikisha Diamond katika wimbo wake wa kwanza alikuwa msanii Akothee akimshirikisha Diamond kwa wimbo wake 'Sweet love'
Ni wimbo ambao una maana nyingi na katika wimbo huo Tanasha anamsihi Diamond asimuache kwa sababu ya wanawake wengine.
Si hayo tu anamwambia Diamond awaambie kuwa yeye ni wake wapende wasipende, huku Diamond akimwambia kuwa mama yake alimwambia simba tulia simba kwa maana ashaampata wa maana.
Hizi hapa hisia tofauti ambazo mashabiki walitoa katika mtandao wa kijamii;
Denogrant
Whoever finds a wife finds a beautiful thing
Bonny Bonny
Diamond is just so talented. He can even just cough and it becomes a big hit.
ESTHER NYOKABI
The only Kenyan Diamond can collaborate with, is his wife… #thesearethefacts🤣
DJ 2ONE2
FACT : – Tanasha in the 2nd Kenyan who has collaborated with Diamond. The first was Akothee – both female. Whatever you do with that info is upto you.
Lilo N.
Diamond and tanasha serving us couple goals wale wa wataachana tu tupige like tukisonga