logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Naomba rais Kenyatta aniruhusu nimuoe Ngina - Rapper Raj

Naomba rais Kenyatta aniruhusu nimuoe Ngina - Rapper Raj

image
na

Habari02 October 2020 - 05:22
rapper raj
Msanii mfokaji (Rapper) kutoka maeneo ya Kisii, Rapper Raj alitangaza kuwa jambo tu moja angetaka kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta ni ruhusa ili aweze kuchumbiana au kumuoa mwanawe.

Raj ambaye amemuimbia Ngina Kenyatta wimbo kwa jina 'Ngina Bae' alisema,

Ningependa kuomba baraka zake, aniambie tu nijitete naweza taka awe sawa na sisi wawili kuwa kwenye mahusiano.

Babangu anaweza furahi sana na isitoshe mamangu ni mcha mungu.

Raj sio mwanaume pekee anaye mmezea Ngina mate. Aprili mwaka uliopita jamaa mmoja kutoka Uchina anayejulikana kama Zhe Fang Liu, ambaye ni mpiga picha alitangaza wazi mapenzi yake kwa kidosho huyo.

Liu ambaye alikuja nchini kutalii, alitangaza upendo wake kwa Ngina licha yake kutowahi patana naye.

Akizungumzia kuhusu mapenzi yake katika mahojiano, Liu alisema,

'Wazazi wangu hushinda wakiuliza ni lini nitaunga pingu za mausha. Swala hilo lilinizidia na nikaamua kuambia watu kuwa nitamuoa Ngina.

Kwa hivyo niliamua kwanza nitampeleka mahali kisha nimpikie chakula cha jioni nione kama sisi wawili tuna mawazo sawa.

Wahenga walisema kuwa urembo wa mwanamke lazima uuone kupitia macho yake kwani hayo ndio malango ya moyo wake.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved