logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Njia 7 za kumgundua ‘gold-digger’

Njia 7 za kumgundua ‘gold-digger’

image
na

Burudani02 October 2020 - 05:28
Woman Holding 100 Dollar Bills
Uhusiano una mambo!  Iwapo hujaoa au kuolewa basi kuna mambo mengi ambayo utayapitia mengine yatakuwa funzo lakini mengine yatakuliza .

Sio wote unaokutana nao na kuanza uhusiano nao wana dhamira kama yako ya kujenga uhusiano  ambao utaishia katika ndoa .Kwa wanaume ,huu hapa mwongozo wa kumtambua mwanamke ambaye hukupendi bali ni ‘gold digger’ yaani yuataka tu hela zako na zawadi unazompa .

  1. Ana uchu sana wa kujua unafanya kazi gani

Ni muhimu ndio kwa mwanamke kujua unafanya kazi gani na wapi .lakini kuwa muangalifu endapo mwenzako ambaye hamjajuana sana anataka kupata undani wa kazi yako na kipato chako . Atakuuliza maswali mengi  kuhusu malipo yako ,manufaa ya kazi yako na vitu vingine ambavyo havihusiani na mnachizungumzia .  Mbinu nzuri ya tangu jadi ya kumtibua  gold digger ni kumdanganya kwanza ..muambie wewe ni shamba boy uone iwapo ataendelea kuwasiliana nawe. Wanawake kama hao ndio huwafanya wanaume kusema wongo ili kuweza kupendwa .unafanya vitu feki ili kujipandisha hadhi machoni  pa mwanamke bila kujua kwamba anakutumia .

  1. Gharama zote ni zako

Wamepatwa na ujanja siku hizi kwamba ni jukumu la mwanamme pekee kugharamia kila kitu . Waangalie hao ambao mkienda hata mkahawani au popote ambapo malipo yatahitajika ,hawaifanya hata kwamba wako tayari kulipa. Watakungoja wewe na mfuko wako utoe kila senti ugharamie hata na starehe zao . iwapo huoni daalili kwamba mwanamke huyo anaweza kuwa msaidizi kwa kuwa tayari hata kukupungumzia mzigo wa gharama hata ndogo basi huyo ni mchimba  dhahabu ..Run!

  1. Anavutiwa na wanaume wa hadhi ya juu .

 Mnawajua ..Hebu jaribu umuambie unaishi   kitongoji cha   bottom line huko Kangemi mashimoni uone iwapo atataka kukuangaliwa mara ya pili. Lakini jaribu umuambie unaishi Loresho au Runda au Karen.Huyoo kakupa namba zake zote hata utapewa  nambari ya next of kin endapo utaipiga simu yake umkose . Kaka iwapo utajipata na huyo basi jua kweli dhahabu imeanza kuchimbwa . Jitayarishe ,piga misuli kasha toka teke!

  1. Zawadi ghali na sasa unaitwa ‘Darling’ na majina yote matamu .

Mletee zawadi za bei ya juu . hapo sasa utakuwa wewe ndio samba ! Ukimpa kitu anachojua bei ama  anachojua kimenunuliwa wapi basi wewe bwege . Vitu vyao vyote kama zawadi lazima view vya kuagizwa kutoka nje . Muahidi utamletea  kipochi kutoka Paris ufaransa na uatafayiwa kila utakacho.Muambie basi   bangili  za kufu zake zitakuwa za dhahabu  na utaitwa ukavyo. Lakini jaribu umpe vyilivyo na wengi mitaani basi utaachwa hapo . Unapompa zawadi,muangalie machoni na utaona usaliti wa macho yake au shukrani ya moyo wake kasha ujiamulie .

  1. Hana maazimio/malengo ya muda mrefu .

 Huyu yuaona kesho na utakavyomnunulia kuku wa kuchomwa na samaki wa kupakwa . Mambo kama  ni wapi au vipi mtakavyojenga nyumba yenu au hata kujiongezea masomo hayapo kabisa katika mipango yake . Utampeleka out lini ndio maswali yake na mbona hujamtumia credit ? mambo yake ni  kesho na kesho kutwa- kuanzia mwezi ujao na mwaka ujao ni wewe na mungu wako .Kaka , huyu uliyempata ni mgeni kumfungia nje .Anza safari ,nunu ganda la avocado na uteleze   kwa kasi yako.

  1. Wewe ndio   jiwe la yeye kupigia hatua moja juu

Iwapo utahisi kwamba mwenzako  anakuhitaji tu ili aweze kuafikia kitu anachotaka  yeye basi fahamu papo hapo kuwa uhusiano huo ni hewa. Anakuambia anakupenda na  muda mfupi wewe kama bosi ushampa kazi au  zabuni na baada ya kupata anachotaka kaput! Uhusiano wenu kwisha .Ashapata alichokitaka na sasa ,anamtafuta mwathiriwa mwingine kwa hatua zaidi za kupanda . Kwani hujasikia mambo ya wanawake ambao wamekitega kweli na wanakitumia kupanda vyeo makazini na hata kuopewa nyongeza ya mishahara? Dunia ina mambo na wewe ni wewe ni mhusika tu .

 

  1. Rafiki zake ni gold diggers .

Umesemwa msemo huu kwamba nionyeshe rafiki zake zako ili nikuambie wewe ni mtu aina gani . Endapo utawajua rafiki zake na uwaone wanavyoendesha mambo yao basi utajua mwenyewe kwamba ngoma hiyo hautaiweza . Wanayosema marafiki wakiwa nawe na hata wakiwa pekee yao ni mambo ambaye yanaweza kutoa ufunuo kuhusu tabia zako na kutoa ufichuzi wa malengo yako .Kaa chonjo basi usije ukapatwa na gold digger ukaachwa hoi kwa sababu hakuna aliyekuambia .

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved