logo

NOW ON AIR

Listen in Live

OMG!Kipusa huyu wa Afrika kusini ashtuliwa na picha yake kwenye chupa

OMG!Kipusa huyu wa Afrika kusini ashtuliwa na picha yake kwenye chupa

image
na

Habari02 October 2020 - 05:28
Mwanadada mmoja kutoka Afrika kusini amewashangaza wanamitandao baada ya kufichua masaibu yake ambapo rafiki wake wa karibu sana  aliichukua picha yake na kuiweka katika chupa .

Mwanadada huyo kwa jina  Asanda Teedow  alionekana kutaka usaidizi wa watumizi wa twitter wamsaidie kujua ni njama ipi rafiki yake alikuwa nayo dhidi yake kwa sababu aliogopa kumuuliza kuhusu vitu hivyo vilivyoonekana kuhusiana na mambo ya ushirikina.Wengi walimtaka aombe kwa sababu huenda rafiki yake hakumtakia mazuri

Tazama ujumbe wake

https://twitter.com/AsandaTeedow/status/1233715828035608576

Asanda anasema alivipata vitu hivyo alipokuwa akichakura ndani ya kabati ya rafiki yake wakati alipokuwa bafuni .

 ‘The reality is, I'm not the only one going through this. Many of you are depressed because your souls are tied to a bottle. So I've decided to share what I've learnt during this experience with you on this video to help’.Ameandika Asanda

  Baadaye alionekana kuwashauri wanamitandao kuwa waangalifu kwa sababu wengi wao huenda pia ni waathiriwa wa mambo ya ushirikina kama yeye na wanahitaji  maombi ..  Amesema hufai kufichua mengi kujihusu kwa rafiki zako na hata jamaa zao . Video yake mtandaoni akieleza masaibu hayo pia aliiweka mtandaoni .

https://twitter.com/AsandaTeedow/status/1234601900642836480

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved