logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond hakuamcha Tanasha bali Tanasha ndiye alimuacha- Tunda wa katibu la umbea

Diamond hakuamcha Tanasha bali Tanasha ndiye alimuacha- Tunda wa katibu la umbea

image
na

Habari02 October 2020 - 09:50
Baada ya Tanasha na Simba kutemana, Tunda wa katibu la umbea akiwa katika mahojiano na Bongo Tosh alizungumzia mambo kadhaa kuhusu uhusiano wa Diamond na mpenziwe Tanasha.

Hii ni baada ya Tanasha kukusanya virago vyake na kurudi humu nchini, alifanya kitendo hicho alipokatazwa kuenda hafla moja nje ya nchi.

Tunda alikuwa na haya ya kusema,

"Tanasha anapost vitu ambavyo anapost kwa maana ameumia sana anajaribu kutoa maumivu moyoni mwake anaelezea kilicho moyoni mwake kupitia post hizo

Kwa kusema ukweli Tanasha hakuwa na upendo kamilifu kwa Simba. Alikuja tu kama wasanii wale wengine ili akuze kipaji chake cha uimbaji

Kwa nini nasema Tanasha kaacha Diamond? Hii ni kwa sababu yeye mwenyewe ndio alijiondoa nyumbani na kuenda hakufurushwa na mtu yeyote." Alieleza Tunda.

Tanasha kutema Simba kulitokea wakati alipost ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram, akisema kuwa Diamond hana heshima na aaminiki kwa chochote.

"Wacha nisema Tanasha alikuwa amekuja kwa Diamond kwa lengo lake alipitia kwa nia ya kimapenzi kukuza muziki, alijisongeza karibu na Diamond ili awe akienda na Diamond kila mahali

Alikuwa anataka aende na yeye ili ajulikane kwenye mataifa yote, ilhali hajasainiwa na lebo la WCB, kitu ambacho mameneja hawajakubaliana nacho." Alieleza Tunda.

Alisema kuwa Tanasha hakufurahishwa na kuachwa na Diamond alipokuwa anaenda katika tour yake ya muziki.

"Hakufurahishwa kabisa, lakini sababu za wimbo wa Diamond na Tanasha kutowekwa katika kurasa za Tanasha

Ni kwa sababu meneja wa WCB washaajua lengo la Tanasha kuwa  na Diamond, mzazi ni mzazi lazima asimame katika lengo lake hata kama uwe nani." Alieleza Tunda.

Kufikia sasa  msanii maarufu  wa nyimbo za bongoDiamond almaarufu Simba hajaweza kuzungumza chochote kuhusiana na tukio hilo alilolifanya Tanasha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved