https://www.instagram.com/p/B-Jk3uRpUSn/
Queen aliyasema hayo katika ujumbe alioambatanisha na picha ya kakake katika akaunti yake ya instagram. Huenda sasa ni rasmi kwamba Simba kweli kaachana na Tanasha Donna kwa sababu dadake anawafungilia wanadada wengine milango katika maisha ya kaka yake.
Katika posti hi ya Insta, dadake mwingine wa Diamond, Esma naye alicheka kwa bezo akisema kwamba huenda akina dada wanamuogopa Kaka yao. Huenda familia ya Diamond ipo nyuma yake kuhusu maamuzi anayofanya ya kuwatema vipusa wote wanaoingia katika maisha yake. Huku wanadada walioathirika wakilalama, dada zake na mamake wameonekana kulichukulia suala zima kama sarakasi na drama!
Mhariri: Davis Ojiambo