logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Habari za Hivi Punde :Mkenya wa kwanza aaga dunia kwa ajili ya Coronavirus

Habari za Hivi Punde :Mkenya wa kwanza aaga dunia kwa ajili ya Coronavirus

image
na

Makala02 October 2020 - 05:58
Jambo Breaking News banner
Kenya imesajili kifo cha kwanza kutokana na virusi vya Corona. Kulingana  na taarifa iliyotiwa saini ya waziri wa Afya Mutahi Kagwe mwanamume mmoja raia wa Kenya mwenye umri wa  miaka 66 ameaga dunia kwa ajili ya virusi hivyo.

Mwanamume huyo  aliyekuwa na ugonjwa wa kisukari pia alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) cha Hospitali ya Aga khan  na alifariki alhamisi alasiri.

Taarifa kutoka kwa wizara ya Afya imesema alikuwa akiugua kisukari na aliwasili nchini tarehe 13 Machi kutoka  Afrika  Kusini kupitia  Swaziland.

Wakati  huo huo kenya imeripoti visa 3 zaidi vya ugonjwa huo nchini na kufikisha 31  watu walioambukizwa Corona hadi kufikia leo.

Wizara ya afya kupitia kwa afisa mkuu msimamizi Mercy Mwangangi  ilithibitisha kuwa taifa la Kenya limesajili visa vitatu zaidi vya Coronavirus na kufanya idadi ya watu walioathirika na virusi hivyo kufikia watu 31.

Wizara hiyo pia ilisema  watu 906 wanaosemekana kukaribiana na waathiriwa wa virusi hivyo  wanasakwa na serikali huku 123 wakiwa wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kufanyiwa vipimo.

Watu 18 nao wamelazwa katika hospitali ya Mbagathi wakisubiri kufanyiwa vipimo na madaktari.

Kaunti ambazo zimeripoti visa hivyo  vya Corona kulingana na wizara hiyo ni; Nairobi, Kilifi, Kwale, Mombasa na Kajiado.

Watatu hao waliopatikana na virusi hivyo wote ni wakenya wawili kutoka kaunti ya Kilifi na mmoja kutoka kaunti ya Nairobi.

Watu zaidi ya 2000 waliofika nchini Jumatatu wameambiwa wajitenga ili kuzuiya kusambaa kwa virusi hivyo kwa watu wengine.

Mhariri: Davis Ojiambo


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved