Diamond alitangaza haya katika video moja alipokuwa akizungumza na mhudumu wa afya na kumuuliza jinsi walivyokuwa wanaendelea na matibabu.
" Kwa mfano kama vile Lizer amepatikana na virusi vya corona, lakini anaonekana mwenye afya na hana shida yeyote itachukua muda gani yeye kupona kabisa na kurudi nyumbani." Diamond Alizungumza.
Akijibu swali la msanii wa bongo alikuwa na haya ya kusema;
"Kirusi cha corona kinaweza kuwa katika mwili wako, mbali uonekane mwenye afya, lakini unaweza kuambukiza waliokaribu na weweCorona ikiisha katika mwili wako ukienda kupimwa tena matokeo yake huwa yanaonyesha kuwa huna kirusi hicho
Baada ya kupimwa huwa unangoja kwa muda wa siku saba kisha unapima tena, kwa hivyo katika kipindi hiki cha karantini kwa siku kumi na nne unapaswa kupimwa mara mbili.
Ukipatikana hauna kirusi hicho hivyo basi utaruhusiwa kwenda nyumbani." Alieleza.
Ni video ambayo ilisambaa sana katika mtandao wa kijamii, licha ya hayo mzalishaji Lizer hajajitokeza na kuzungumzia hali yake ya afya.