logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Steven Kanumba: Mfalme wa flamu za bongo aliyeaga dunia katika hali ya kutatanisha

Steven Kanumba: Mfalme wa flamu za bongo aliyeaga dunia katika hali ya kutatanisha

image
na

Michezo02 October 2020 - 06:11
Tarehe 7 Aprili  mwaka wa 2012 itasalia tarehe ya kuzua machungu kwa mamilioni ya mashabiki wa muigizaji maarufu wa filamu kutoka Bongo marehemu Steven Kanumba.

Kifo chake katika hali ya kutatanisha   akiwa nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam bado kinajadiliwa hadi leo hasa siku hii ambapo kumbukizi  ya kifo chake inaadhimishwa. Kanumba  alipata umaarufu na kuibuka kama muigizaji balozi wa filamu za Kiswahili katika Tanzania na afrika mashariki.Wakati wa mazishi yake, maelefu ya watu waliyahudhuria na hata rais Jakaya kikwete aliahirisha safari yake nje ya nchi ili kwenda kumzika msanii huyo. Mamia ya watu pia walisafiri kutoka maeneo ya Bunia na Kisangani,mkatika Jamhuri ya DRC kwenda kumzika Kanumba .

Awali ilidaiwa  Kanumba alifariki baada ya  kugombaa na muigizaji  mwenzake Elizabeth Michael aka Lulu . Lulu baadaye alihukumiwa jela kwa mwaka mmoja na kuachiliwa. Alidai Kanumba alijaribu kumshambulia kwa panga na kumfanya kuanguka hadi akazirai.B aadaye alipopata fahamu alitoroka kuokoa maisha yake lakini akaarifiwa kwamba Kanumba alikuwa ameaga dunia .

Steven Kanumba alizaliwa mwaka 1984 na anatajwa kuwa ni mmoja wa waigizaji walioitambulisha na kuikuza sanaa hiyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Maudhui ya filamu zake na umaarufu wake ulimfanya kupendwa kote Afrika, na kisa chake cha kupanda hadi kilele cha utajiri kutoka familia maskini pia kilikuwa kama jambo la kuwapa wengi matumaini .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved