logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nimezoea masimango! Paul Pogba aambia wanaomsema sema

Nimezoea masimango! Paul Pogba aambia wanaomsema sema

image
na

Habari02 October 2020 - 06:23
NA NICKSON TOSI

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amesema hababaishwi na semi za kila mara kutoka kwa wachambuzi wa soka Uingereza na kwamba amezoea matamshi yao ya kila mara kumhusu.

Mchezaji huyo wa Ufaransa ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Uingereza akitokea klabu ya Italia Juventus mwaka 2016, alicheza mechi yake ya mwisho kabla ya kupata jeraha mnamo disemba mwaka jana dhidi ya Newcastle mechi ambayo walisajili ushindi wa magoli 4-1.

Miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakimsema kiungo huyo ni mchezaji wa kitambo wa klabu ya Liverpool Graeme Souness ambaye alimtaja kiungo huyo kama mtu mnafiki inapowadia wakati wa kucheza.

Aidha mchezaji huyo alikwa anatarajiwa kushirikishwa katika mechi za hivi karibuni za klabu ya Manchester United, japo kutokana na virusi vya Corona ligi hiyo ilisitishwa kwa muda.

Alikuwa anauguza jeraha la kinena baada ya kufanyiwa upasuaji na madaktari.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved