Tecra Muigai, binti yake mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Keroche breweries Tabitha Karanja amefariki katika ajali ya barabara.
Kulingana na taarifa ya kampuni hiyo, Tecra alifariki jana baada ya kuhusika katika ajali wakati wa mchana. Tecra ambaye alikuwa binti yake Tabitha na mwenyekiti wa Keroche Joseph Karanja alikuwa kiongozi wa mikakati na uvumbuzi katika kampuni hiyo.
Kwingineko, kaunti ya Mombasa imefutilia mbali gharama za wakaazi ambao walikuwa kwenye kwarantini. Katika taarifa iliyotolewa Jana, idara ya afya ya kaunti hiyo ilikubaliana na taasisi hiyo ya kutoa mafunzo ya udaktari na kuwachilia watu 38 ambao walikuwa wamewekwa kwenye kwarantini katika taasisi hiyo.
Hilo lilifanyika siku kadhaa baada ya wagonjwa kulalama kuwa kuwa hawawezi pata shilingi elfu ishirini na nane za kulipa taasisi hiyo baada ya mda wao wa kwarantini kutimia.
Hayo yakijiri, mwanaume mwenye umri wa miaka 30 amekamatwa katika kaunti ya Homa Bay kwa kumdhulumu kingono msichana mwenye umri wa miaka kumi anayeugua ugonjwa wa kifafa.
Mwanaume huyo alimdhulumu msichana huyo siku ya Ijumaa akiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Otaro.
Inaripotiwa kuwa alijaribu kumshawishi msichana huyo wa gredi ya kwanza kwa kumpa shilingi 150 na kuamua kumfanyia unyama huo alipokataa.