logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Makahaba wageukia mifumo ya dijitali kuuza bidhaa zao

Makahaba wageukia mifumo ya dijitali kuuza bidhaa zao

image
na

Habari02 October 2020 - 07:08
prostitutes_421217179-696x351
Taaluma ya jadi sana duniani, ukahaba sasa imeanza kuendeshwa kwa njia ya dijitali. Ukiwa mteja sasa unaweza kumpata mhudumu kwa tuvuti au kwa app.

Hata hivyo, makahaba wazee bado hawajaanza kutumia mifumo ya dijitali kunadi mizigo yao na wanadai kuwa ni vigumu kupata wataalam wa kuwatengenezea tuvuti.

Biashara ya ukahaba nchini Kenya ina changamoto chungu nzima kwa sababu hapa nchini kufanya ukahaba ni hatia katika sheria za nchi.  Lakini licha ya haya yote biashara hiyo bado imenoga huku wanawake kwa wanaume wote wakiuza miili yao ili wapate senti.

Ukahaba wa dijitali umeanza kupata umaarufu katika maeneo ya jiji la Narobi na miji mingine mikuu nchini Kenya. Alex ambaye hutoa huduma za ngono kwa wanawake na wanaume wanaozihitaji anasema kwamba ameweza kushughulikia mahitaji ya familia yake katika mtaa wa Lovington kupitia kazi hii.

"Natafutia wanasiasa na wateja wengine matajiri wanawake warembo. Nimekuwa katika biashara hii kwa miaka mitano na najuana na wengi. Kila wakati warembo wabichi wanapoingia ulingoni mimi hupashwa habari,” alisema.

“Wanawake hunitumia picha zao wakiwa uchi na mimi huzituma kwa rafiki zangu kwa kundi letu la mtandao wa kijamii ambalo mimi ndiye msimamizi na tunahudumia mtu kulingana na ombi lake. Yule anayependa mwanamke huniambia faraghani na tunakubaliana malipo.” Alieleza.

Yeye hutoza kati ya shilingi 5,000 kwenda mbele kulingana na mwili wa mwanamke. Akiwa mnene malipo yanaongezeka.

Mwandishi wetu alijifanya kahaba na kutembelea eneo moja hapa Nairobi ambalo shughuli za ukahaba huendeshwa. Ilimbidi amlipe shilingi 50 mama anayesimamia shughuli za ukahaba katika eneo hilo na kumnunulia bia mbili ili aruhusiwe kutega katika eneo hilo.

Danguro hilo ni mojawapo ya madanguro katikati ya jiji la Nairobi eneo la River road.

Katika madanguro ya River road, makahaba hukaa nje kwa baridi wakisubiri wateja na kuwashawishi kila mara 'mwanamume anapopita'.

Mwandishi wetu akiwa katika eneo hilo, mwanamume mmoja kwa jina Steve alimkaribia na kuomba ampe shot moja kwa shilingi 200, lakini yeye alimwambia alete 500, na mwanamume huyo akaeda zake akisema kwamba bei yake ilikuwa ghali mno.

Alipouliza kama angeruhusiwa kusajiliwa kuwa mwenyeji katika danguro hilo, alipewa masharti makali.

Meneja wa danguro hilo alimwambia,

"Unafaa kupiga picha ukiwa uchi ili zitumike kwa tuvuti yetu, ulete kitambulisho chako na vipimo vya HIV". 

Jukwaa za dijitali za kuuza ngono zimefanya biashara ya ukaba kuwa rahisi kwa malaya wengi kupata wateja na wateja kupata makahaba kwa urahisi.

Ukiwa wewe ni mteja wa biashara hii haya basi uamuzi ni wako 'unataka dijital au unataka analogue'


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved