Mama huyo wa watoto wanne amesema amekuwa akilipa kodi hiyo tangu kuhamia kwa nyumba hiyo Desemba japo mambo yalibadilika baada ya serikali kufunga shughuli nyingi nchini.
“Nimekaa hiyo miezi yote wa nne sasa ndio landlord anaona sifai kwa sababu kazi sasa imedidimia, mimi nauzaga mitumba ambayo sasa watu hawanunui kwa sababu hawajui zimetoka nchi gani,” amesema Shiundu.
Jaribio lake la kutakata kupata usaidizi limegona mwamba hata baada ya kujaribu kumfikia chifu wa mtaa huo japo hakuna usaidizi ambao ameupata.
“Aliniambia tarehe kumi mwezi huu lazima niwe nimemlipa nilipokosa nikamwambia sijapata akaniambia sitaweza na siwezi kuvumilia ndio akaja na caretaker wake na grinder akakata mlango wote,” Ruth amesema.
Mwanawe kijana Nevili aliongeza kwa kusema
“Deni ile ambayo tuko nayo ni ya miezi miwili tukiwa kwa do jana ndio huyu dadangu alipiga simu akasema caretaker wamepanda huko juu na ngazi wanatoa paa tukifika hapa tukapata imeharibika. Alisema Nevili.
Kulingana na mamlaka ya takwimu za kitaifa yaani Kenya National Bureau of Statistics kupitia kwa ripoti yao ya Jumanne, asilimia 30.5 ya wakenya hawangeweza kulipa nyumba Aprili kutokana na mkurupuko wa corona.
Asilimia 21.5 ya wakenya hawana uwezo wa kujikimu kimaisha .
Huku asilimia 59.8 ya wakenya wakiwa na uwezo wa kulipa nyumba kama walivyokubaliana na mmiliki wa nyumba.
