logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alidhani albamu yetu haitafana! Ethics na Octopizzo wajibizana

Alidhani albamu yetu haitafana! Ethics na Octopizzo wajibizana

image
na

Michezo02 October 2020 - 07:38
Ethic--1024x681
Majibizano baina ya wanamuziki wa kikundi cha Ethics na msanii wa hip hop nchini Otopizzo yanazidi kuibua hisia mseto baada ya Ethics kudai kuwa Octopizzo alikataa kushirikishwa katika albamu yao akidhani haitafanya vyema .

Kupitia mtandao wao wa twitter, Ethics waliandika kuwa Khaligraph Jones anafanya vyema kuliko Octopizzo, semi ambazo zilimpelekea Octo kujibu kuwa ni kutokana na hatua yake ya kukataa kushirikishwa katika albamu ya wasanii hao.

“Aaah is it because I refused to jump on your project or? Anyway, it is life. Wakiritho TA!TA!” Octopizzo alisema

Ethics walilazimika kujibu madai hayo kati yao.

“We gave @OCTOPIZZO the privilege to be on our super dope album but hakuona vision, truth ni numbers ziko but ange kuja tu na zile mathogothanio zake, video for the song wasn’t part of the plan…all in all watch out June 13th album dropping, ‘BIG MAN BADO ODINARE’ Ni mbwaya ni moto” Ethic waliandika

Ethics aidha siku za hivi maajuzi wamekuwa wakikashifiwa na wakenya kutokana na nyimbo zao kuwa za uzushi haswa zinazozungumzia maswala kuhusiana na ngono kila mara..


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved