Akiwa kwenye mahojiano, Otile alisema kuwa huwa anafanya hivyo ili kuwa mwaminifu katika uhusiano wake na mpenzi wake Nabayet almaarufu Nabbi.
“Tunanyonga tu! Utafanya nini sasa! Nikimsubiri na anasupport mnyongo huo, anasema keep doing what you are doing. Anajua with that now, at least boy wake nimetulia." Otile Alisema.
Hivi maajuzi, Otile alitoa albamu mpaya ya 'just in love' akiwa kwenye mahojiano alisema kuwa mpenzi wake huwa hapiki endapo atamtembelea, bali huwa anapika na hata kumlisha Nabayet.
"Mpenzi wangu hajawahi pika akija kunitembelea unajua watu wengi hawanijui vyema katika maisha yangu ya maabara ya mapenziMimi ndo napika na amekaa tu hapo kwa sababu ni mimi nimechagua kufanya hivyo, unajua hajawahi shika chakula na mkono huwa namlisha
Na si wala nimekaliwa chapati, nimechagua kufanya hivyo kwa maana nampenda sana mwanamke huyo. Naona kuna mafisi wengine huku nyuma wanatoa tu gangster points." Alizungumza Otile.
Akizungumzia uhusiano wake na Nabayet, alisema kuwa ni wapenzi na uvumi ambao ulitokea kuwa wameachana walisuluhisha makosa yao.
“My last relationship, vitu vilitokea na wanawake wakanielewa kwamba, I’m ruthless, mimi ni mtu ambaye ikifika kwa mademu sijatulia. So when we first got into the relationship, she wasn’t sure about, like it did not matter how much I tell her nakupenda, and thats why I went and sang Nabayet, whatever I sang on Nabayet is all true. Because I don’t think I have ever loved a woman, the way I love that chick, coz ni mwanamke ambaye hana story mingi. She will never bother you. She that type of a woman ukimkosea atalia, she will just cry. So it was always a struggle, like so many times we are having the same discussion. Any time I tell her I really care about you , I love you anasema No you are just playing with me." Alieleza.
Nabayet kwa sasa anaishi mjini Australia, lakini humtembelea Otile mara kwa mara mjini Nairobi.