logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Battle for supremacy! Auma Obama amkashifu Malik Obama kwa kumuone gere Barack Obama

Battle for supremacy! Auma Obama amkashifu Malik Obama kwa kumuone gere Barack Obama

image
na

Habari02 October 2020 - 07:55
Untitled-design-43
Cheche za maneno sasa zimeanza kushamiri baina ya familia ya Obama baada ya Auma Obama kumkashifu nduguye Malik Obama kujaribu kumharibia sifa rais wa zamani wa Amerika Barack Obama kwa kujaribu kutuma cheti feki cha kuzaliwa kwenye mtandao wa Twitter.

Auma ameelezea kusikitishwa na tukio hilo na kusema Malik anafanya hivyo kutokana na wivu baada ya Barack Obama kuwa rais wa Amerika.

Malik alikuwa ametundika cheti ghushi kilichokuwa kinaonyesha tarehe ya kuzaliwa kwa Barack Obama kilichoonyesha kuwa kiongozi huyo wa zamani wa Amerika alizaliwa Agosti mwaka 4,1961 katika hospitali kuu ya Coast General Mombasa, Jamhuri ya Kenya.

Wakenya katika mitandao ya kijamii almaarufu kama KOT, waligutushwa na kukejeli cheti hicho na kudai kuwa taifa la Kenya lilifahamika kama Jamhuri ya Kenya mwaka 1964 bali si 1961 kama ilivyokuwa imeandikwa kwa cheti hicho.

Wengine walibaini kuwa msajili aliyekuwa ametia saini katika cheti hicho hakuwa wa humu nchini bali kilikuwa kimeandikwa Australia.

Auma kama njia ya kumjibu vyema Malik, alisema amekuwa akiishi na machungu haswa baada ya Barack Obama kuwa rais wa taifa la Amerika.

Malik is consumed and driven by jealousy and bitterness towards President Obama “that you will go to any length to slander your younger brother’s name-literally.” Just because he has outshone you in every single aspect of his life. Seek relevance elsewhere big brother,”alisema Auma Obama

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved