logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pastor Kanyari :Nimechoshwa na hatua ya Betty Bayo kutajataja jina langu mitandaoni

Pastor Kanyari :Nimechoshwa na hatua ya Betty Bayo kutajataja jina langu mitandaoni

image
na

Habari02 October 2020 - 08:41
Msanii wa nyimbo za Gospel Betty Bayo amejipata pabaya na aliyekuwa mume wake na baba ya watoto wake Pator Victor Kanyari ambaye sasa amejitokeza kulaani hatua ya Bayo kulitajataja jina lake katika kumbi za mitandao ya kijamii.

Betty amekuwa akifunguka kila mara kuhusu makosa aliofanya kujiingiza katika uhusiano na  Kanyari.Amekuwa akikumbuka mateso aliyopitia na unafiki wa mhubiri huyo lakini Kanyari sasa amesema amechoshwa na tabia hiyo na Betty anafaa kuwa na ujasiri wa kuachana naye na kuendelea na maisha yake.

Kanyari ameshangaa ambona Betty humtaja yeye tu ilhali aliwahi kuwa na wapenzi wengine kabla hajakutana naye anaofaa pia kuwataja katika sarakasi zake za mitandaoni. Wengi  wameonekana kumshauri Kanyari kwamba Betty yungali anampenda ndio maana anada inakuwa vigumu kuacha kuzungumza kumhusu lakini Kanyari amesema katu hawezi kurudiana na mama ya watoto wake wawili .

“She should not be worried that I may appear and fight for love. I am a good man and I don’t fight for love. I have never been with a person I loved that much to make me fight for her to love me. When we separated, it’s a decision we made so I cannot go back to her,”  alisema

Kanyari pia alipinga madai kwamba alikuwa na mazoea ya kumpiga Betty walipokuwa katika ndoa yao

 “I never hit her when we were together. The fact remains we separated. I never touched her. One day I came home angry and hit a picture on the wall but I never fought her. She can even testify to that.”

Ushauri wake kuhusu mapenzi ukatamatishwa kwa sentensi hii

“Ukiachwa achika. Otherwise, depression is there. If she was not your destiny, then let her go and stop begging for their love. If she stays, it’s okay,”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved