Kupitia ujumbe aliounakili kwenye mitandao ya kijamii ya instagram Akothee aliweka wazi kuwa gharama ya hospitali italipwa na bima yake na kama haitatosha kulipa mali yake itauzwa ili gharama hiyo ilipwe.
Pia alinakili kuwa mtu yeyote asijaribu kutengeneza 'paybill' ya kulipa mazishi yake au mchango wa mazishi yake kwa maana amepanga hayo yote.
"Familia ni familia ata nikiwa kwenye kitanda changu cha kifo, dada yangu mkwe alizikwa kama sikuwa kwa maana nilikuwa napigana na maisha yangu katika hospitali ya KarenLakini nililipa kila kitu nilikuwa inahitajika nilinunua nguo na hata jeneza la mazishi, sina wazo lolote kwa nini nisiweze jilipia gharama yangu ya hospitali
Na hata kushughulikia wengine mimi ni nani mwanamke asiyejijali
Kama vile nilivyowaambia awali, nina bima ya hospitali nimekata bima kwa ajili ya mtoto wa dada yangu na mama yangu bima haingeweza kukata baba yangu kwa ajili ya umri wake
Niko sawa kulipa gharaa yake ya hospitali kutoka kwa mfuko wangu, kwa hivyo kama haya yote yamisha na nibaki bila pesa tafadhalini uzeni mali yangu niweze kuzikwa
Jeneza langu tayari limeshughulikiwa, cha mwisho pia nina bima ya mazishi mtu yeyote atakaye kuja na mpango wa paybill ili nizikwe itakuwa ni kashfa." Aliandika Akothee.
Jeneza langu tayari limeshughulikiwa, cha mwisho pia nina bima ya mazishi mtu yeyote atakaye kuja na mpango wa paybill ili nizikwe itakuwa ni kashfa." Aliandika Akothee.
