Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kwamba mvua inatarajiwa kuendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya nchi katika kipindi cha siku saba zijazo.
Maeneo hayo ni nyanda za juu magharibi mwa bonde la Ufa, Eneo la Lake Victoria, Kati na Kusini mwa bonde la ufa na Kaskazini mashariki.
Soma habari zaidi;
Baadhi ya maeneo yakiwemo Elgeyo-Marakwet, Nandi, Laikipia, Nakuru, Narok, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma na Busia yanatarajiwa kushuhudia vipindi vya jua majira ya asubuhi.
Nyanda za juu mashariki mwa bonde la Ufa ikiwemo Nairobi na baadhi ya maeneo ya Kusini mashariki mwa nyanda za chini na kati na kusini mwa bonde la ufa zinatarajiwa kushuhudia hali ya kibaridi na mawingu.
Maeneo mengi ya Kaskazini mashariki, ukanda wa Pwani na kusini mashariki mwa nyanda za chini zinatarajiwa kusalia kavu.
Maeneo ya Kaskazini Mashariki (Marsabit, Mandera, Wajir, Garissa na Isiolo) yanatarajiwa kuwa na jua majira ya mchana na mawingu nyakati za siku.
Soma habari zaidi;
Vile kesi ya Monicah Kimani iliua kazi ya Jacque Maribe
Manyunyu yanatarajiwa kushuhudiwa siku moja moja katika baadhi ya maeneo.
Kajiado, Kitui, Makueni, Machakos na Taita Taveta zinatarajiwa kushuhudia jua mchana na mawingi mepesi nyakati za usiku
Maeneo ya kaskazini magharibi (Turkana, West Pokot na Samburu) yatapokea mvua nyakati za asubuhi na alasiri huku ngurumo za radi zikitarajiwa pia.
Hali hii ya hewa ni kati ya Agosti 3-9.