Amekuwa mstari wa mbele kupigania haki na usawa humu nchini na pia ameyapitia mazito katika maisha yake .
“ Nampeza sana mke wake alikuwa jaji mzuri sana’ ameliambia gazeti la The Star . Joyce Khaminwa ,mke wake wa miaka 48 aliaga dunia mwaka wa 2014 katika Nairobi Hospitali .alikuwa jaji wa mahakama kuu wakati huo .
“ Naam , tulikuwa na ndoa nzuri sana kwa miaka 48 .alikuwa mtu mzuri sana’ amesema Khaminwa huku huzi ikitanda wazi usoni mwake .Huenda kfo kilimpokonya ndoa aliyoijenga kwa nguvu na hali zote .
Dr Khaminwa ana jingine pia la kumpa huzuzi anapozungumzia kifo cha mwnawe wa kwanza Albnert Khaminwa aliyeaga dunia mwaka wa 2017 akimtaja kama mmoja wa waliofuata nyayo zake kwa kuwa wakili . Albert alikuwa amefika kiwango chakuwa mshirika katika kampuni yao ya uanasheria ya Khaminwa & Khaminwa Advocates.
“ Alikuwa mtoto mwerevu sana’ wakili huyo anasema huku ikionekana wazi kwamba vifo vya wapendwa hao wake wawili vimeacha pengo kubwa sana katika maisha yake .
Anakaribia kugonga miaka 84 na ameshuhudia vitu vingi sana vingine vilivyomsadia na vingine havijamchangia chochote katika maisha yake .Kinachomtoa mawazo ni kuendelea kufanya kazi yake ya uwakili kwa miaka 50 hadi sasa .Kazi hiyo yake ndio inayomfanya kuamka kila siku na kutojawa na mawazo kuhusu vitu vingi vinavyofanyika katika maisha yake .
“ kuwa wakili ni jambo la kipekee .napenda sana kusikiliza matatizo ya watu ,inaniondoewa mawao’ amesema
Khaminwa anapenda sana sheria na hayuko tayari kustaafu anasema ni kifo pekee kitakachomzuia kuendelea na kazi ya uwakili .
Dr Khaminwa amewaakilisha watu wenye majina tajika wakati wa taaluma yake iliyodumu nsu ya karne huku baadhi ya kesi zikimletea uhasama na rais mstaafu Daniel Moi na hata akajipata amefungwa jela .
“ Nimewaakilisha Raila, Matiba, George Anyona miongoni mwa wenine katika mapambanao dhidi ya utawala wa kiimla’ anasema Khaminwa . Hatua yake ya kumwakilisha Stephen Mureithi, aliyekuwa amehamishwa kama naibu mkuu wa idara ya ujasusi ni hatua ambayo ilimhamakisha sana rais Moi
Kesi nyingine tajika aliyoishughulikia ni ilyohusisha utata wa kimila kati ya ukoo wa Umira Kager kutoka Alego dhidi ya Wambui Otieno ambaye alitaka mwili wa mume wake SM Otieno kuzikwa nyumbani kwao Ngong Matasia mwaka wa 1986. SM Otieno alikuwa wakili tajika enzi hizo na Dr Khaminwa alimwakilisha mjane Wambui
Khaminwa alishinda raundi ya kwanza wakati mahakama kuu ilipoagiza mjane kupewa mwili ili auzike Ngong lakini ukoo huo ukashinda kesi baada ya kukata rufaa na mwili ukapelekwa Alego ,Siaya
Ilikuwa mojawapo ya kesi zilizochukua muda mrefu –zaidi ya mwaka mmoja huku mwili wa SM Otieno ukisalia katika hifadhi ya maiti ya City
