logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siri ilivyotoka ya Mapenzi kati ya Mwalimu na Mwanafunzi-Masaibu!

Siri ilivyotoka ya Mapenzi kati ya Mwalimu na Mwanafunzi-Masaibu!

image
na

Yanayojiri01 October 2020 - 09:46
Teacher
Kuna mahusiano ambayo hayawei kukubalika na jamii kwa sababu yanakiuka sharia na pia maadili ya utendakazi . Amesimulia kisa mwalimu mmoja wa shule ya upili aliyependana na mwanafunzi wake  na wakati ufichuzi ulipotolewa kuhusu penzi hilo ,jamaa alipoteza kazi yake baada ya kuhamishwa kwenda shule ambayo hangeweza kwenda kuifunza .

Mwalimu Fred alikuwa akifunmza somo la hesabu na kemia katika shule  moja ya wasichana . kwa sababu ya ujana wake  ,aliwavutia wanafunzi wake wengi wa kike hasa wa vidato vya tatu na nne ambao wengine walikuwa na ujasiri wa kutisha kwa kumuandikia vibarua vya mapenzi na kauviweka katika  vitabu vyao ili akutane  navyo wakati anapovisahihisha . Taaluma yake ya ualimu haikuwa imedumu hata miaka mitatu wakati alipohamishwa hadi katika shule moja ya wasichana ambako pia mwalimu mkuu alimpa majukumu ya kuwa mwalimu wa  michezo ya kuigiza . Pale ikawa anatangamana sana na wanafunzi wake hata nje ya shule wakati wanapokwenda katika shule jirani kwa mashindano ya drama .

Haikuwa mpango wake kumpenda mwanafunzi wake lakini alivutiwa na mmoja wa watahiniwa wa KCSE mwaka huo ambaye alikuwa na macho ya kuvutia sana . Mwalimu alijaribu kujizuia lakini mwanafunzi wake hakuwa na kithibiti na moyo ukaslimu  amri  muda mfupi baadaye wakaanza uhusiano huo haramu . Mwanafunzi alimpa hakikiso mwalimu kwamba  ni miezi mitatu tu ambapo  atakuwa mwanafunzi kwa sababu pindi baada ya mtihani wa KCSE angemaliza masomo ya shule ya upili na pale  sasa uhusiano wao ungeuwa wa mtu mzima kwa mwingine . Jambo ambalo hawakuwa wamelipangia ni kwamba  Fred alikuwa amejenga chuki sana na wanafunzi wengine wa kike ambao hawakupendezwa na hatua yake ya kuwapuuza na badala yake kuamua kujiingiza katika uhusiano na mwanafunzi huyo mmoja wa kidato cha nne ambaye  mara nyingi alionekana naye na hata Fred alikuwa  akimpa mafunzo ya ziada ili kumwezesha kufanya vyma katika mtihani wa KCSE .

Ile kamato ya roho chafu ilikuwa na hila dhidi ya mwalimu Fred na walipanga njama ya kulitibua penzi na mtu na mwalimu kwa kuandika barua ambaypo haikuwekwa jina la mwandishi na kuitupa katika afisi ya mwalimu mkuu . Katika barua hiyo walidai kwamba Mwalimu Fred alikuwa na mazoea na tabia ya kuwatongoza wanafunzi wake . Hilo lilizua mheko shuleni kwani wale ambao hawakujua ukweli wa mambo walichukulia madai hayo kama ukweli halisi . Mwalimu  Fred alitakiwa kuchukua likizo ili  uchunguzi ufanywe na baadaye ilipobainika kwamba ni kweli alikuwa na uhusiano na mwanafunzi wa kidato cha nne alihamishwa hadi eneo la Tana River ambako hakuweza kwenda . Fred aliamua kuacha taaluma ya ualimu kwa sababu katika barua yake ya uhamisho iliandikwa kwamba alifaa kuchungwa sana asiwakaribie  wanafunzi wa kike na hilo lilimpaka doa aisweze kuaminiwa na yeyote hata alipokuwa akihamishiwa .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved