Wanajeshi wa KDF siku ya Jumatatu waliwaua wanamgambo watano wa kundi la kigaidi la Alshabaab walipojaribu kuvamia msafara wa KDF.
Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la Lafey, Kaunti ya Mandera karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.
Huku maafisa wa idara ya usalama wakidinda kujibu maswali kuhusu tukio hilo, duru za kuaminika zilisema kwamba afisa mmoja wa KDF aliuawa huku wengine wawili wakijeruhiwa wakati wakijaribu kukabiliana na wapiganaji wa Alshabaab.
Duru zasema kwamba magaidi walishambulia msafara wa KDF kwenye barabara ya Angu-Elwak wakitumia magruneti na bunduki nyakati za asubuhi.
Inasemaka wanajeshi wa KDF walikuwa safarini kuelekea kiwanja cha ndege waliposhambuliwa na kupulekea makabiliano makali.
Mbali na wapiganaji watano waliouawa wengi waliroka na majeraha ya risasi.
Kisa hiki kimetokea siku tano tu baada ya wafanyibiashara wawili waliokuwa kwenye pikipiki kushambuliwa na washukiwa wa Al Shabaab katika barabara ya Fino-Sheikh kaunti ndogo ya Lafey.