Kamati ya kusimamia utekelezaji wa katiba inayoongozwa na Jermiah Kioni imesema ilikuwa makosa kwa maraga kulishtumu bunge kwa kukosa kutekeleza sharia ya usawa wa kijinsia ilhali hata idara ya mahakama haijatekeleza kanuni hiyo .
Awali tume ya utumishi kwa bunge PSC ilisema itachukua hatua ya kupinga ushauri wa Maraga kwa rais Kenyatta .
Mwenyekiti wa PSC spika wa bunge Justin Muturi amesema ushauri huo haufai ni unakiuka katiba .
Amesema tume hiyo inajutia kwamba jaji Mkuu anatishia kulitumbukiza taifa katika mgogoro wa kikatiba bila kutumia busara na heshima ya afsisi yake.
Muturi siku ya jumatatu alisema bunge halifai kufanywa bagi la kupigwa makonde akisema sio jambo linalowezeka kumtaka rais alivunjie mbali bunge kwa kukataa kuteleleza sharia ya usawa wa kijnsia