Kylian Mbappe na Cristiano Ronaldo wote walishindwa kufunga mabao wakati washindi hao wa kombe la dunia na mabingwa wa Uropa kutoka sare tasa jijini Paris.
Kiungo wa Juventus Ronaldo hakufunga bao na anasalia kuwa na mabao 101 katika mechi za kimataifa, Ureno waliposhindwa kurudia ushindi wao wa Uro mwaka 2016 ugani Stade de France. Mbappe alitarajiwa kuwa fursa bora zaidi ya Ufaransa kufunga kwa ujuzi wake, lakini juhudi zake zikazuiwa na kipa Rui Patricio. Mechi hio ilishabikiwa na zaidi ya mashabiki elfu moja wa Ufaransa.
Uingereza ilitoka nyuma na kuinyuka Ubelgiji 2-1 na kurekodi ushindi muhimu katika Nations League ugani Wembley. Ubelgiji walichukua uongozi wa awali, wakati Romelu Lukaku alimpomchenga kipa wa Uingereza Jordan Pickford na kutia bao kimyani.
Uingereza walionyesha mchezo mzuri kunako kipindi cha kwanza cha mechi hio na kuongezewa matumaini wakati nahodha Marcus Rashford alipofunga bao la ufunguzi. Vijana wa Gareth Southgate wakatawala mechi baada ya mapumziko lakini walihitaji bahati kubwa ili kupata ushindi, huku bao la Mason Mount likimpita kipa Simon Mignolet na kupelekea Ubelgiji kupoteza kwa mara ya kwanza tangu Novemba mwaka 2018.
Italia ilisalia kileleni mwa Kundi A1 katika Nations League baada ya kutoka sare dhidi ya Poland huko Dansk.
Kikosi cha Roberto Mancini bado hakijashindwa na wako alama moja juu ya Uholanzi, ambao walitoka sare ugenini na Bosnia awali. Nyota wa Poland Robert Lewandowski hakuonyesha mchezo mzuri kwani hakuweza hata kupiga mkiki mmoja karibu na lango.
Mlinzi wa Chelsea Emerson Palmieri alipoteza nafasi kubwa kwa Italia katika kipindi cha pili, akiunganisha pasi ya Federico Kiesa karibu na lango la Lukasz Fabianski, wakati krosi ya Leonardo Bonucci ilimnyima Karol Linetty ushindi kunako dakika za lala salama. Mwishowe pande zote mbili zilikosa ushindi na wanafika nusu ya hatua za vikundi na alama moja tu ikiwatenganisha.
Hayo yakijiri, pendekezo la kubadilisha mfumo wa kupiga kura wa ligi ya Primia, na vilevile mifumo ya ufadhili ya ligi ya Uingereza EFL na FA, limetungwa na wamiliki wa Liverpool na linaungwa mkono na Manchester United. Pendekezo hilo lijulikanalo kama Project Big Picture linajumuisha mabadiliko mengine makubwa kwa mfumo wa soka ya Uingereza, ikiwemo kupunguzwa kwa timu kutoka 20 hadi 18 katika ligi ya Primia, na kufutiliwa mbali kwa kombe la EFL na Community Shield.
Mazungumzo ya awali kati ya Liverpool, United na vilabu hivyo vingine sita vikubwa, Manchester City, Tottenham, Arsenal na Chelsea yamefanyika, huku kukiwa na matumaini kuwa watakubaliana.
Kwingineko, Lewis Hamilton aliiifikia rekodi ya ushindi katika Formula1 kwa kushinda Eifel Grand Prix. Ushindi wa dereva huyo wa Mercedes ulikuwa wa 91 katika tajriba yake na ana uhakika wa kuvunja rekodi ya Michael Schumacher hivi karibuni.
Hamilton aliongezea uongozi wake wa ubingwa dhidi ya Valtteri Bottas hadi alama 69 baada ya raia huyo wa Finland kujiondoa. Nyuma ya Max Verstappen wa Red Bull kwa sekunde, Daniel Ricciardo alifunga jukwaa la kwanza la Renault tangu arejee kwa F1 kama mjenzi mnamo 2016. Mbio hizo zilikuwa zinatarajiwa kuwa kinyangányiro kati ya Hamilton na Bottas kabla ya gari la pili la Mercedes kupata matataizo huko Ujerumani.